Pata taarifa kuu
DRCongo-Mapigano

Zaidi ya watu arobaini wapoteza maidha katika mapigano ya jana mjini Kamango mashariki mwa DRCongo

Takriban watu arobaini wamepoteza maisha hapo jana katika mapigano yaliozuka kwenye kijiji cha Kamango mashariki mwa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo. Mashirika ya kiraia katika eneo hilo yamethibitisha kuwa yamehesabu miili ya watu Arobaini ambao wote ni raia wa kawaida waliouawa na kundi la waasi waliovamia kijiji hicho wakitokea nchini Uganda.

Wanajeshi wa DRCongo katika mji wa Kamango
Wanajeshi wa DRCongo katika mji wa Kamango Irinnews
Matangazo ya kibiashara

Duru kutoka katika eneo hilo zimearifu kwamba mapigano hayo yalikuwa makali na waasi hao walikuwa wamejihami vya kutosha na silaha, waliofaulu kuuteka mji huo kwa muda kadhaa kabla ya kufurushwa.

Shirika la msalaba mwekundi linaendesha uchunguzi kutafuta iwapo kuna miili ya watu wengine waliopoteza maisha kwenye mapigano hayo. Kiongozi wa shirika la kiraia katika mji wa Beni Teddy Kataliko amesema watu wengine zaidi ya kumi wamejeruhiwa katika mapigano hayo.

Hapo jana watu watu kumi walitekwa, na wengine kumi na moja raia wa kawaida na wanajeshi watano wakajeruhiwa, huku wananchi wengi wakipoteza maisha na majumba kadhaa kuteketezwa kwa moto.

hapo jana asubuhi watu wenye silaha waliuvamia mji wa Kamango na kuuteka, kabla ya majeshi ya serikali yaliosaidiw ana wanajeshi wa Umoja wa Mataifa kushambulia waasi hao waliotoroka mji huo baada ya kutekeleza mauaji.

Mashirika ya kiraia katika mkoa wa Kivu ya Kaskazini yamethibitisha kuwa waasi hao walishambuliao raia wa mji wa Kamango ni wa kundi la Uganda la ADF-NALU ambao walishirikiana na majeshi, taarifa ambayo haikuthibitishwa na upande wowote.

Hata hivyo kumekuwa na taatifa kwamba waasi hao ni wa kundi la M23 ambao wamerejea tena upya wakiwa wamejizatiti vya kutosha na kuanzisha tena uasi.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.