Pata taarifa kuu
KENYA

Bunge nchini Kenya lapitisha muswada tata wa ndoa, wanaharakati waupinga

Wabunge nchini Kenya wamepitisha muswada tata kuhusu ndoa, ambapo wanandoa watakapotalakiana watagawana mali yao kwa misingi ya mchango wa kila mmoja katika kusaka mali hiyo wakati wakiwa pamoja.

Bunge la nchini Kenya
Bunge la nchini Kenya RFI
Matangazo ya kibiashara

Muswada huo ambao umepingwa vikali na wabunge wanawake pamoja na kutoungwa mkono na wanawake wengi nchini Kenya umepokelewa kwa hisia tofauti na wanaharakati wa ndoa ambao wanadai muswada huo unalenga kumgandamiza mwanamke.

Awali sheria ya ndoa ilitaka wanandoa kugawana mali sawa kwa sawa pindi watakapotalakiana jambo ambalo pia halikuwapendeza sana wanaume ambao wanadai kwa sehemu kubwa ndio hushiriki kuchangia pakubwa mali wanazomiliki.

Muswada huo uliibusha malumbano makali ndani ya bunge la nchi hiyo ambapo wabunge wakiume walihoji iweje walipe mahari na gharama nyingine wakati wa mchakato wa kuoa halafu mwisho wa siku wakija kuachana wagawane mali sawa kwa sawa.

Kauli hiyo ikapingwa vikali na wabunge wanawake ambao nao wanatetea upande wao wakisema muswada huo unaendelea kuweka mambo ya mfumo dume ili kumnyima haki mwanamke.

Muswada huo sasa utawasilishwa kwa rais ili atie saini na kuwa Sheria.

Zaidi mwandishi wetu wa Nairobi ana mengi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.