Pata taarifa kuu
Syria-mkutano

Hatma ya kikao cha Giniva kuhusu Syria ipo mashakani baada ya upinzani kugawanyika, huku shirika la msalaba mwekundu likitiwa hofu na kutekwa kwa wafanyakazi wake

Waziri wa mashauriano na nchi za nje wa Marekani Johna Kerry anakutana na mjumbe  maalum wa Umoja wa Afrika nchini Syria Lakhar Brahimi kwa ajili ya kuandaa mkutano wa Giniva Uswisi mwezi ujao kuhusu Syria. Taarifa hii inakuja wakati kukiwa na mpasuko katika baraza la kitaifa nchini Syria huku upinzani ukiendelea kugawanyika na huenda muda wa kufanyika kwa mkutano huo ukarefushwa.  Shirika la kimataifa la msalaba mwekundu ICRC limesema litanedelea na shughuli zake za kutowa huduma nchini Syria na kwamba swala la Usalama wa wafanyakazi wake linapewa kipao mbele. Taarif hii inakuja saa kadhaa baada ya kutekwa kwa wafanyakazi wake 6 na mmoja wa shirika la mwezi mwekundu raia wa Syria.  

kingozi wa baraza la upinzani kitaifa nchini Syria
kingozi wa baraza la upinzani kitaifa nchini Syria AFP PHOTO / OZAN KOSE
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huo wa baraza la kitaifa CNS nchini Syria wa kutoshiriki katika mkutano wa pili wa Giniva unajiri wiki tatu baada ya Ahmad al Assi al-Jarba kiongozi wa muungano wa makundi ya uasi nchini humo kutangaza nia yake ya kushiriki kwenye mkutano huo.

Matukio haya yanaonyesha kiasi gani upinzani nchini Syria ulivyogawanyika hasa kufuatia mkanganyiko ulipo baina ya wafadhili wakuu wa wapinzani hao Saudia Arabia na Uturuki.

Katika hatuwa nyingine, Shirika la kimataifa la msalaba mwekundu ICRC limesema litanedelea na shughuli zake za kutowa huduma nchini Syria na kwamba swala la Usalama wa wafanyakazi wake linapewa kipao mbele. Taarif hii inakuja saa kadhaa baada ya kutekwa kwa wafanyakazi wake 6 na mmoja wa shirika la mwezi mwekundu raia wa Syria.

Msemaji wa shirika hilo la ICRC Ewan Watson akiwa jijini Uswisi amesema, tukio hilo haliwezi kamwe kuwakatisha tamaa ya kuendelea kutowa huduma kwa wananchi wa Syria wanaohitaji misaada kwa wakati huu, lakini ni tukio ambalo linawapa fursa ya kutafakari kuhusu swala la Usalama ambapo amesisitiza hawawezi kuendelea na shughuli hiyo bila kutilia maanani usalama wa wafanyakazi wao.

Ewan Watson amejizuia kutowa uraia wa wafanyakazi hao waliotekwa lakini wengi wao ni raia wa Syria.  wafanyakazi hao walitekwa kwenye mji wa Idlib ambapo watu wenye silaha walishambulia msafara wake uliokuwa ukirejea mjini damascus huku kundi lililowateka likidai walikuwa wanashirikiana na makundi ya kigaidi.

Msemaji  huyo wa shirika la kimataifa la msalaba mwekundu amesema wanatiwa hofu na matukio kama hayo ambayo yanaweza kuwazuia kuendelea kutekeleza shughuli zao kama ipasavyo katika siku zijazo na ametowa wito wa kuachiwa huru kwa wafanyakazi hao bila masharti yoyote

Wakati hayo yanajiri, Umoja wa mataifa UN hapo jana umemtangaza Sigrid Kaag kama kiongozi wa ujumbe wa umoja huo ulioko nchini Syria kwa kushirikiana na jopo la wataalamu waliopewa jukumu ya kuteketeza silaha za kemikali.

Uteuzi wake unakuja wakati huu ambapo kumeripotiwa mapigano kwenye miji kadhaa nchini humo pamoja na shambulio la bomu la kujitoa muhanga mjini Damascus ambapo watu kadhaa wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.