Pata taarifa kuu
BANGLADESH

Mahakama maalumu nchini Bangladesh yamuhukumu kunyongwa katibu mkuu wa chama cha Jamaat e-Islam

Mahakama moja nchini Bangladesh imemuhukumu kunyongwa katibu mkuu wa chama cha upinzani cha kiislamu nchini humo baada ya kumkuta na hatia ya kushirikia mauaji ya mwaka 1971 wakati wa vita na Pakistan. 

Wafuasi wa chama cha Jamaat e-Islam wakiandamana juma hili kupinga hukumu dhidi ya viongozi wa chama chao
Wafuasi wa chama cha Jamaat e-Islam wakiandamana juma hili kupinga hukumu dhidi ya viongozi wa chama chao Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mahakama ya kimataifa iliyoundwa nchini humo kusikiliza kesi za viongozi wa zamani walioshiriki mauaji ya wakati wa vita vya uhuru dhidi ya Pakistan imeamuru kunyongwa kwa Ali Ahsan Mohammad Mujahid.

Mahakama hiyo ambayo imekosolewa kwa sehemu kubwa na wanaharakati nchini humo imemkuta na hatia ya makosa matatu kati ya makosa matano aliyokuwa anashtakiwa nayo.

Mujahid ambaye ni mtu wa pili wa juu mwenye madaraka kwenye chama cha Jamaat e-Islam anakuwa kiongozi watatu kuhukumiwa na mahakama hiyo baada ya juma hili kumuhukumu kifungo cha miaka 90 aliyewahi kuwa mwenyekiti wa chama hicho Ghulam Azam.

Kesi hizo dhidi ya viongozi wa chama cha Jamaat kimeligawa taifa hilo kwakuwa wanapinga mauji hayo wanataka viongozi wote waliohusika na mauaji kuhukumiwa kunyongwa huku wafuasi wa chama hicho wakiona kesi hizo zimechochewa kisiasa.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.