Pata taarifa kuu
MAREKANI-URUSI

Marekani yaitaka Moscou kushirikiana nayo katika shughuli za kumsafirisha Edward Snowden

Serikali ya Marekani imeiomba Moscou kushirikiana nayo katika shughuli za kumsafirisha nchini Marekani mfanyakazi wa zamani wa kituo cha intelijensia cha Marekani CIA Edward Snowden ili kujibu tuhuma dhidi yake.

Edward Snowden mfanyakazi wa zamani wa CIA
Edward Snowden mfanyakazi wa zamani wa CIA
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa usalama wa taifa nchini Marekani caitlin Hayden amefahamisha kuwa kutokana na ushirikiano wa mataifa hayo mawili ulioimarika tangu kutokea kwa mlipuko jijini Boston wakati wa mbio za Marathon, Pamoja na utekelezwaji wa usafirishaji wa wahalifu wakuu, kuna matumaini makubwa kuona serikali ya Urusi inamfukuza Edward Snowden nchini Marekani ili akapambane na mahakama.

Msemaji huyo wa idara ya usalama nchini Marekani amesema kusiktishwa na hatuwa ya serikali ya Hong kong ya kumuacha Snowden kuelekea nchini Moscou licha ya ombi halali la Marekani la kutaka kukamatwa kwake kama unavyoruhusu mkataba wa ushirikiano baina ya mataifa hayo mawili.

Hayden amesema wamewasilisha ujumbe wa lamawa kwa Hong kong na serikali ya China kupitia njia za kidiplomasia na kufahamisha kuwa uamuzi kama huo unaweza kuathiri kwa kiasi kikubwa uhusiano uliopo kati ya Marekani na Hong Kong na Marekani na China.

Snowden, anatafutwa na Marekani kwa kuvujisha taarifa za siri dhidi ya taifa hilo kuwa inafuatilia shughuli za ki elektroniki, aliwasili Jumapili nchini Moscow akitokea Hong Kong, ambako amekimbilia na sasa anatafuta hifadhi ya kisiasa nchini Ecuador.

Marekani imekuwa ikitaka kuhodihwakwa hati yake ya kusafiria na kuomba mfanyakazi huyo wa zamani wa CIA na Shirika la Usalama wa Taifa (NSA) kuzuiliwa kundelea na safari yake.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.