Pata taarifa kuu
VATICAN

Mjadala waanza kuhusu mrithi wa Papa Benedicto wa 16

Baada ya kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Benedicto wa 16 kutangaza siku ya Jumatatu kuwa atajiuzulu tarehe 28 mwezi huu kutokana na umri wake mkubwa na kukosa nguvu za kuendelea kuongoza kanisa hilo, mjadala umeanza kuhusu ni nani atakayemrithi.

Matangazo ya kibiashara

Wachambuzi wa mambo ya uongozi katika Kanisa hilo wanasema kuwa wakati umefika kwa kanisa hilo kupata Papa ambaye anatoka nje ya bara la Ulaya baada ya John Paul kutoka Poland na Benedicta wa 16 kutoka Ujerumani kuwa viongozi wa Kanisa hilo kwa muda mrefu.

Kiongozi mpya wa kanisa hilo atapatikana mwezi ujao baada ya uchaguzi utakaofanywa na Makadinali kabla ya Sikukuu ya Easter mwezi Aprili  katika makao makuu ya Kanisa hilo mjini Vatican nchini Italia.

Eneo la Marekani ambalo lina asilimia 42 ya Wakatoliki wote duniani linaona kuwa wakati umefika kwa kiongozi mpya wa Kanisa hilo kutoka eneo hilo huku Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Sao Paolo Odilo Scherer, akipewa nafasi kubwa ya kumrithi Papa Benedicto wa 16.

Peter Turkson kutoka Ghana ambaye anaongoza idara ya haki na amani katika Kanisa hilo pia anapewa nafasi kubwa kuwakilisha bara la Afrika kama kiongozi mpya wa kanisa hilo.

Kujiuzulu kwa kiongozi huyo kumetokea ghafla na kuwashangaza waumini wa Kanisa hilo duniani.

Papa Benedicto mwenye umri wa miaka 85 alisema hawezi tena kuhudumu kama kiongozi wa Kanisa hilo ambalo amekuwa akiongoza tangu mwaka 2005 baada ya kufariki kwa Papa John Paul wa pili.

Kujiuzulu kwa kiongozi wa juu wa Kanisa Katoliki duniani ni jambo ambalo halijawahi kutokea katika historia ya Kanisa hilo na hii ndio mara ya kwanza, huku viongozi watano waliopita wakifia madarakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.