Pata taarifa kuu
MAREKANI

Hillary Clinton awa mbogo mbele ya wabunge wa Congress kuhusu shambulio la Benghazi nchini Libya

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani anayemaliza muda wake, Hillary Clinton ametetea kile ambacho kilitkelezwa na Serikali yake katika kushughulikia ghasi zilizotokea kwenye ubalozi wake mjini Benhazi nchini Libya mwaka jana ambapo balozi wake na raia wengine watatu waliuawa. 

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Hillary Clinton akijibu swali wakati akihojiwa na wabunge wa Congress
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Hillary Clinton akijibu swali wakati akihojiwa na wabunge wa Congress REUTERS/Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

Akiongea kwa hasira wakati wa mahojiano yake na wabunge wa Congress toka chama cha Republican, Clinton amewashutumu wabunge hao kwa kulifanya suala la Benghazi kama ajenda yao ya kisiasa wakati wanajua fika kuwa Serikali ilichukua hatua stahiki katika kuahikisha matukio kama hayo hayajirudii.

Waziri Clinton ameongeza kuwa hakukuwa na upotoshaji wakati wa utolewaji wa taarifa kuhusu tukio hilo na kwamba taratibu zote zilifuatwa katika kuhakikisha kunakuwepo taarifa sahihi.

Seneta wa Republican Ron Johson aliendelea kumuuliza waziri Clinton ni kwanini Serikali yake ilihusisha tukio lile na tukio la kigaidi lililotekelezwa na kundi la Al-Qaeda.

Katika kujibu swali hilo waziri Clinton amesema kuwa tukio lile hata kama halikuwa na uhusiano na mtandao wa kigaidi lakini bado lilikuwa ni tukio la kinyama ambalo ni watu ambao wanamsimamo mikali na itikadi za makundi ya kigaidi ndio waliolitekeleza.

Katika mahojiano hayo wakati mmoja waziri Clinton alitokwa na machozi wakati akieleza namna ambavyo Serikali ya rais Barack Obama ilivyohakikisha inakuwa karibu na familia za ndugu waliopoteza maisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.