Pata taarifa kuu
KAMPALA-UGANDA-DRC

Hakuna dalili ya kupatikana muafaka kwenye mazungumzo ya Kampala kati ya waasi wa M23 na Serikali ya DRC

Mazungumzo baina ya Kundi la Waasi la M23 na Viongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC yameendelea kukabilia na vikwazo huku daliliza wazi zikijionesha hakutakuwa na muafaka wa dhati. 

Mwakilishi wa waasi wa M23 kwenye mazungumzo ya Kampala Roger Lumbala
Mwakilishi wa waasi wa M23 kwenye mazungumzo ya Kampala Roger Lumbala REUTERS/James Akena
Matangazo ya kibiashara

Kikwazo kipya kwenye mazungumzo hayo ni madai ya Waasi wa M23 kutaka suala la uhalali wa serikali ya Rais Joseph Kabila wa Kabange lijadiliwe kutokana na wengi kusema haikuchaguliwa na raia wengi.

Kwa mujibu wake Crispus Kiyonga waziri wa ulinzi na msuluhishi wa mazungumzo hayo anasema kuwa sio jukumu lake kuingilia taasisi na serikali ya DRC ambayo ilichaguliwa na wananchi,na kaongeza kuwa viongozi wa mataifa ya maziwa makuu waliomba suala hilo lisiweze kuguswa.

Kauli hiyo iliwagawanya wajumbe wa M23 miomngoni mwao wakajitoke za wale ambao walidhihirisha kuwa tayari kujiondoa kwenye mazungum zo hayo,huku wengine wakisema kuwa tayari hadi tamati.

Serikali ya Kinshasa kupitia msemaji wake Lambert Mende imeelezea kuridhika kwake na msimamo huo,na kusema kuwa kinachotakiwa kujadiliwa kwa undani ni makubaliano pekee yaliyosainiwa Mjini Goma mnamo marchi 23 2009.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.