Pata taarifa kuu
Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Nchi za SADC zatangaza utayari wake wa kupeleka Jeshi nchini DRC huku Mazungumzo baina ya Waasi wa Seleka na Serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati yakiendelea Gabon

Imechapishwa:

Mataifa wanachama wa SADC watoa vikosi vyao kuunda Jeshi Huru la Kimataifa ambalo litapelekwa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kulinda maeneo yanayoshikiliwa na Waasi wa M23, Mahakama ya Rufaa nchini Burundi yampunguzia adhabu mwandishi wa habari Hassan Ruvakuki toka adhabu ya kifungo cha maisha jela na kuwa miaka mitatu, Waasi wa Seleka waendelea kuvutana na Viongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati katika kufikia suluhu ya kufanyika mabadiliko ya serikali kwenye mazungumzo yao huko Gabon na Rais wa Marekani Barack Obama aendelea na uteuzi wa mawaziri kabla ya kuapishwa kuiongoza nchi hiyo kwa awamu ya pili!!!

Viongozi kutoka nchi Wanachama za SADC wakiwa kwenye Mkutano wa kujadili hali ilivyo nchini DRC, Madagascar na Zimbabwe
Viongozi kutoka nchi Wanachama za SADC wakiwa kwenye Mkutano wa kujadili hali ilivyo nchini DRC, Madagascar na Zimbabwe
Vipindi vingine
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.