Pata taarifa kuu
KENYA-SOMALIA

Shambulio la Guruneti lasababisha vifo vya watu wawili katika kambi ya wakimbizi mpakani mwa Kenya na Somalia

Watu wawili wameauwa na wengine kadhaa kujeruhiwa kufuatia shambulizi za guruneti jana ijumaa katika kambi ya wakimbizi mashariki mwa Kenya karibu na mpaka wa Somalia. Polisi nchini humo wamethibitisha kutokea kwa shambulio hilo la jana ijumaa.

raxanreeb.com
Matangazo ya kibiashara

Shirika la msalaba mwekundu nchini humo limesema wawili waliokufa ni vijana na wengine watu saba wamejeruhiwa vibaya katika shambulio hilo lililotekelezwa katika kambi ya Daadab iliyopo takribani kilometa 100 toka katika mpaka wa Somalia.

Mashambulizi ya mara kwa mara yamekuwa yakishuhudiwa nchini Kenya tangu serikali ya nchi hiyo kupeleka wanajeshi wake kukabiliana na wapiganaji wa Al Shabaab mwishoni mwa mwaka 2011.

Bado wapiganaji wa Al Shabaab wanaendelea kumiliki eneo kubwa la kusini mwa Somalia licha ya vikosi vya Umoja wa Afrika AMISOM, Kenya na Ethiopia kukabiliana nao katika baadhi ya miji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.