Pata taarifa kuu
Morocco

Marafiki wa Syria wakutana mjini Marrakesh Morocco kuunga mkono upinzani

Wajumbe kutoka zaidi ya mataifa 100 yanayojiita marafiki wa Syria wanakutana mjini Marrakesh nchini Morocco kutambua baraza jipya la upinzani nchini Syria kama wawakilishi wa wananchi wa taifa hilo, siku moja baada ya Marekani kusema pia inalitambua baraza hilo la upinzani.

Matangazo ya kibiashara

Rais Barrack Obama amesema baraza hilo sasa limeonesha ulimwengu kuwa linawakilisha wananchi wote wa Syria na kuwalinda dhidi ya uongozi wa rais Bashar Al Assad.

Mbali na Mareakani, mataifa mengine ambayo tayari yametambua baraza hilo ni pamoja na Uingereza, Ufaransa, Uturuki na mataifa ya muungano wa nchi za Ghuba.

Obama amesema sasa baraza hilo la upinzani lina jukumu la kuhakikisha kuwa haki za watu wa zinazingatiwa na kushirikiana na jumuiya ya kimataifa kuona namna ya kulisaidia baraza hilo kupambana vilivyo na uongozi wa rais Assad.

Hata hivyo, Marekani inaonya kuwa haitawaunga mkono wala kusaidia makundi ya kigaidi ndani ya baarza hilo la upinzani.

Machafuko nchini Syria yameendelea kwa mwaka wa pili sasa kati ya wapinzani wa rais Assad na wanajeshi wa serikali na mashirika ya kutetea haki haki za binadamu yanasema makabilinao hayo yamebabaisha vifo vya watu zaidi ya elfu 40 kwa kipindi cha miezi 18 iliyopita.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.