Pata taarifa kuu
EGYPT-CAIRO

Watu kadhaa wameripotiwa kufa kwenye maandamano nchini Misri nje ya makazi ya rais Morsi, ulinzi waimarishwa

Jeshi la Misri limepeleka vifaru na magari ya kivita nje ya makazi ya rais wa nchi hiyo Mohamed Morsi ikiwa ni hatua ya kuimarisha ulinzi kutokana na maandamano ya wananchi ambao wamezunguka makazi yake. 

Maelfu ya wananchi wa Misri wakiandamana nje ya makazi ya rais Morsi
Maelfu ya wananchi wa Misri wakiandamana nje ya makazi ya rais Morsi Reuters
Matangazo ya kibiashara

Usiku wa kuamkia leo kumeshuhudiwa makabiliano makali kati ya polisi na waandamanaji ambao wamezunguka makazi ya rais wakishinikiza kiongozi huyo kujiuzulu ama kubatilisha uamuzi wake wakujilimbikizia madaraka makubwa.

Watu watatu wameripotiwa kupoteza maisha kwenye vurugu za kuamkia usiku wa leo ambapo wengine zaidi ya mia nne wameripotiwa kujeruhiwa kutokana na makabiliano na polisi.

Polisi wa kutuliza ghasia wamelazimika kutumia mabomu ya machozi na risasi za mpira kuwatawanya maelfu ya waandamanaji waliozingira makazi ya rais ingawa bado wanakabiliwa na upinzani toka kwa waandamanaji hao.

Hapo jana baadhi ya wafuasi wa rais Morsi walikabiliwa na waandamanaji wanaompinga kiongozi huyo kwenye maandamano ambayo tayari yameleta hali tete ya kisiasa nchini Misri.

Hapo jana taarifa kutoka ikulu ya nchi hiyo imesema kuwa mshauri wa masuala ya siasa wa rais Mohamed Morsi alitangaza kujiuzulu kutokana na machafuko yanayoendelea.

Viongozi wa madhehebu ya Suni nchini humo wamewataka wananchi kurejesha hali ya utulivu nchini humo wakati huu Serikali ikushughulikia suala la katiba mpya.

Upinzani nchini humo unapinga muda uliotengwa kwa majaji kupitia rasimu ya katiba wakidai kuwa hautoshi na pia bunge lilivunja kanuni kwa kuteua watu wachache toka cha cha Muslim Brotherhood kupitia rasimu hiyo na kuipitisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.