Pata taarifa kuu
UFILIPINO

Idadi ya vifo kutokana na mafuriko nchini Ufilipino yaendelea kuongezeka

Idadi ya watu waliokufa kutokana na mafuriko yaliyoikumba nchi ya Ufilipino imeendelea kuongezeka na sasa imeelezwa idadi yao kufikia watu zaidi ya 200 huku wengine mamia hawajulikani walipo.

Mmoja wa wananchi wa Ufilipino akiwa amezungukwa na maji na tope
Mmoja wa wananchi wa Ufilipino akiwa amezungukwa na maji na tope Reuters
Matangazo ya kibiashara

Vikosi vya uokoaji nchini humo vimeendelea kukabiliana na hali mbaya ya hewa ambayo imeendelea kuikumba nchi hiyo huku maeneo mengi yakiwa hayafikiki kutokana na miundombinu yake kuharibiwa na mafuriko na maporomoko ya udongo.

Mamia ya wananchi hawajulikani walipo kutokana na nyumba nyingi hasa kwenye mji wa Mindanao kufunikwa na vifusi vya udongo pamoja na maji huku nyingine zikiwa zimeezuliwa paa kutokana na upepo mkali.

Kimbunga cha Bopha kinaelezwa kusafiri kwa kasi ya kilometa 210 kwa saa hali inayofanya zoezi la uokoaji kuwa gumu zaidi kutokana na kuzidi kwa upepo ambao unakwamisha zoezi hilo.

Kitengo cha maafa nchini humo kimesema kuwa hali inazidi kuwa mbaya nchini humo kutokana na kuendelea kuongezeka kwa idadi ya watu waliokufa kutokana na mafuriko huku wakiomba jumuiya ya kimataifa kusaidia watu walioathirika.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.