Pata taarifa kuu
COLOMBIA-FARC

Wanajeshi wa Colombia waua wapiganaji 20 wa kundi la waasi wa FARC kwenye mpaka wake na Ecuador

Kundi la Waasi la nchini Colombia la FARC linakabiliwa na tarehe ya mwisho ya kusitisha kugomea mazungumzo ya amani ambayo yanafanywa na serikali baada ya Rais Juan Manuel Santos kutoa onyo la kufikiwa kwa makubaliano baina ya pande hizo mbili. 

Wapiganaji wa kundi la FARC nchini Colombia mabo Serikali imeshambulia kambi zao
Wapiganaji wa kundi la FARC nchini Colombia mabo Serikali imeshambulia kambi zao Reuters
Matangazo ya kibiashara

Onyo hili dhidi ya Kundi la Waasi la FARC linakuja kipindi hiki ambacho wanajeshi wa Serikali ya Colombia wakibainisha kutekeleza operesheni ilisababisha vifo ishirini vya waasi hao mwishoni mwa juma.

Kundi la FARC limetakiwa kukaa mezani na kuafikiana na serikali ili kumaliza vita iliyodumu kwa miongo mitano katika taifa hilo kitu ambacho kimetajwa kulemaza shughuli za maendeleo.

Waasi wa kundi la FARC wamesema hawatarejea kwenye meza ya mazungumzo na Serikali ya Colombia kwa kile walichoeleza kukiuka makubaliano ya kustisha mashambulizi yake dhidi ya waasi hao.

Viongozi wa kundi hilo wamesema kuwa hivi karibuni wataanza kujibu mashambulizi dhidi ya wanajeshi wa Serikali ikiwa ni pamoja na kuanza utekelezaji wa utekaji nyara kwa raia wa kigeni nchini humo.

Iwapo mazungumzo hayo yatagonga mwamba basi huenda nchi hiyo ikashuhudia vita kati ya serikali na waasi wa FARC ikiendelea kwa miaka mingine zaidi iwapo hakutapatikana muafaka.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.