Pata taarifa kuu
JAPAN

Serikali ya Japan yaagiza kufanyika uchunguzi wa kina kuhusu ajali ya njia ya ardhini mjini Sasago, mashariki mwa Tokyo

Serikali nchini Japan imetangaza kufanyika uchunguzi wa kina kuhusu sababu zilizopelekea kuanguka kwa paa la njia ya ardhini na kisha kuwaka moto ambapo watu tisa wameripotiwa kupoteza maisha.

Vikosi vya uokoaji vya Japan wakiwa kwenye eneo la tukio kujaribu kuingia ndani ya barabara ambayo paa lake lilianguka siku ya Jumapili na kuua watu tisa
Vikosi vya uokoaji vya Japan wakiwa kwenye eneo la tukio kujaribu kuingia ndani ya barabara ambayo paa lake lilianguka siku ya Jumapili na kuua watu tisa Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kwenye taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari nchini humo imesema kuwa waziri wa ardhi, miundombinu, usafiri na Utalii ameagiza kufanyika kwa uchunguzi wa kina kubaini chanzo cha tukio hilo.

Mwishoni mwa juma njia ya ardhini inayounganisha mji wa Tokyo mashariki mwa nchi hiyo paa lake lilianguka na kufunika magari yaliyokuwa yakipita kwa wakati huo na kisha kuwaka moto.

Njia hiyo iko umbali wa kilometa 80 toka mji wa Tokyo na imekuwa ikitumika muda mrefu bila ya kuwa na hitilafu yoyote mpaka siku ya jumapili ambapo paa lake lilianguka na kufunika magari.

Tayari vyombo vya habari vimeeleza kuundwa kwa tume maalumu kuchunguza ajali ya sasago na kutakiwa kuwasilisha matokeo yake kwa serikali kulingana na muda ambao wamepewa kutekeleza jukumu hilo.

Hii inaelezwa kuwa ni ajali mbaya zaidi ya njia ya ardhini kuwahi kuikumba sekta ya usafiri nchini Japan ambapo pia tume hiyo imetakiwa kuchunguza miundo mingine ya ardhini ili kuifanyia tathmini.

Uchunguzi wa awali umeonesha huenda nguzo ambazo zilikuwa zinashikilia paa hilo zilikuwa zimeharibika na hivyo kushindwa kuhimili uzito na kisha kuanguka.

Nchi ya Japan inazidi ya miundo mbinu ya barabara za ardhini zaidi ya 20 ambayo pia imedumu kwa miongo kadhaa na hivyo kuzua hofu kuhusu uimara wa miundo mbinu hiyo ambayo watu wameshauri kufanyiwa ukarabati.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.