Pata taarifa kuu
Syria

Syria yaituhumu Marekani kuunga mkono magaidi

Syria inaituhumu Marekani pamoja na washirika wake kwa kuendelea kuunga mkono ugaidi nchini humo kwa kuwahami na kuwafadhili wapiganaji wanaotaka kuuangusha utawala wa rais Bashar Al Assad.

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa mambo ya nje wa Syria Walid al-Moualem amesema serikali yake inashangazwa na hatua hiyo ya Marekani ya  kuunga mkono makundi ya kigaidi  nchini mwake huku akisisitiza kuwa serikali yake iko tayari kwa mazungumzo ya kisiasa ili kumaliza mapigano yanayoendelea.

Mualem amewaambia wajumbe katika mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani kuwa nchi yake imekuwa ikikabiliana na makundi ya kigaidi yanayoungwa mkono na mataifa ya kigeni tangu kuanza kwa mapambano nchini mwake mwaka uliopita.

Marekani na Ufaransa zimeendelea kusisitiza mabadiliko ya uongozi nchini Syria huku Qatar, Saudi Arabia na Uturuki wakiaminiwa na Syria kuwa wanawafadhili waasi hao kwa silaha na fedha.

Mashambulizi yanayoongozwa na majeshi ya Syria yameendelea kuwashambulia waasi katika mji wa Allepo na kusababisha vifo vya raia wasiokuwa na hatia wakiwemo watoto.

Mapigano dhidi ya rais Bashar Al Assad yameingia katika mwezi wa kumi na tisa na kusababisha mauaji ya zaidi ya watu elfu 30 na maelfu kujeruhiwa.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.