Pata taarifa kuu
AFRIKA MASHARIKI

FAO yaonya kuhusu mashambulizi ya nzige Afrika Mashariki

Shirika la Chakula na Kilimo FAO, linaonya kuwa nzige walio Kusini mwa Ethiopia wanaanza kusambaa kuelekea katika mataifa ya Afrika Mashariki.

Nzige
Nzige REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

FAO katika ripoti yake ya hivi punde, inasema nzige hao wameanza kuonekana Mashariki mwa Ethiopia na baadhi ya maeneo ya Somalia, kuelekea Kaskazini Mashariki mwa Kenya.

Tayari nzige hao wapo katika kaunti za Kenya za Wajir, Garisa na Marsabit  lakini wenine wameonakana katika kaunti ya Taita Taveta, karibu na Tanzania.

Shirika hilo linaonya kuwa, kuendelea kuwepo kwa nzige hawa kunatishia usalama wa chakula katika eneo la Afrika Mashariki, baada ya mwaka uliopita, nchi hizo za Afrika Mashariki kuharibu Mabilioni ya wadudu hao.

Tayari nzige hao wameonekana katika Wilaya ya Mwanga, Kaskazini Mashariki mwa Tanzania na FAO inaonya kuwa iwapo hatua za dharura hazitachukuliwa, huenda hali ikawa mbaya katika siku zijazo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.