Pata taarifa kuu
KENYA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Kenya yaendelea kukabiliwa na ongezeko la maambukizi

Kenya imeripoti maambuzi mapya Elfu moja na nane, ya maambukizi ya Corona, huku watu 21 wakipoteza maisha, ikiwa ni idadi kubwa kuwahi kuripotiwa kwa kipindi cha saa 24 zilizopita, ongezeko ambalo linalokuja siku moja baada ya rais Uhuru Kenyatta kutangaza hatua mpya za kukabiliana na janga hilo.

Kenya imeendelea na juhudi za kuzuia kuenea kwa Corona.
Kenya imeendelea na juhudi za kuzuia kuenea kwa Corona. REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Rais Kenyatta, sasa ameongeza muda wa makataa ya watu kutembea usiku hadi Januari 3, hii ni baada ya taifa mwezi Octoba pekee, kurekodi maambukizi mapya elfu 15 na vifo zaidi ya 300.

Septemba 28 mwaka huu, Serikali yake ilitangaza kulegeza makataa zilizokuwepo, ambapo saa za makataa ya kutembea usiku ziliongezwa kwa saa mbili na shule kuruhusiwa kufunguliwa kwa awamu.

Mwezi uliopita pia, wizara ya afya, ilieleza kuguswa kutokana na kurejelewa kwa mikutano ya kisiasa, iliyosema inaongeza hatari ya maambukizi, mikutano ambayo sasa, rais Kenyatta ameipiga marufuku na kuruhusu ile ya ndani peke yake.

Katika hatua hizi mpya za Serikali, watu ambao watakutwa hawajavaa barakoa watakamatwa na sekta za umma na binafsi zimetakiwa kutotoa huduma kwa raia ambao hawatakuwa na barakoa.

Hadi kufikia Novemba 3, Kenya ilikuwa na jumla ya maambukizi elfu 53 na vifo zaidi ya elfu 1.

Uchumi wa taifa hilo umeathiriwa pakubwa kutokana na janga la Corona, hasa sekta za huduma za jamii, utalii, biashara pamoja na usafiri, huku mamilioni ya watu wakipoteza ajira.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.