Pata taarifa kuu
TANZANIA-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Tanzania: Upinzani waonywa kutothubutu kufanya maandamano, wapinzani kadhaa wakamatwa

Rais wa Tanzania John Magufuli amekabidhiwa cheti cha ushindi na Tume ya Uchaguzi baada ya kutangazwa wiki iliyopita, kupata asilimlia 84 ya kura, katika zoezi ambalo wapinzani wamedai kulitokea udanganyifu mkubwa, huku Marekani nayo ikitilia shaka matokeo hayo.

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli.
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli. REUTERS/Sadi Said
Matangazo ya kibiashara

Aidha, Rais Magufuli amesema wakati wa kufanya siasa umekwisha.

Vyama vikuu ya upinzani nchini humo ACT-Wazalendo na CHADEMA vimetaka wafuasi wake kuanza maandamano yasiyo na kikomo kuanzia leo, kupinga matokeo ya uchaguzi huu.

Hata hivyo baadhi ya taarifa zinabaini kwamba Baadhi ya viongozi wa upinzani nchini Tanzania wanashikiliwa na polisi baada ya kutangaza kupanga maandamano ya amani leo Jumatatu ili kuonesha kutokubaliana na matokeo ya uchaguzi.

Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha CHADEMA Freeman Mbowe pamoja na aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema na aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es Salaam Boniface Jacob wako mikononi mwa vyombo vya usalama kwa mujibu wa polisi.

Viongozi hao wa upinzani walipanga kuhatarisha usalama wa raia kwa kufanya vurugu kuonyesha kutokubaliana na matokeo. Watu hao wanapanga kuingia mtaani kuchoma maeneo mbalimbali kama masoko, magari na vituo vya mafuta, amesema Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa.

Hayo yanajiri wakati katika visma vya Zanzibar, rais mteule Hussein Ali Mwinyi anatarajiwa kuapishwa leo Jumatatu kama rais rasmi wa visiwa hivyo.

Siku ya leo ni mapumziko Zanziibar ili kuwaruhusu watu wote waweze kushiriki kwa ukamilifu sherehe hizo.

Wakati huo huo Kamanda wa polisi mkoa wa mjini magharibi ameta onyo kali pia kwa viongozi wa vyama vya upinzani vya ACT-Wazalendio na CHADEMA kutoandamana na yeyote atakayejitokeza hawata sita kumchukulia hatua kali za kisheria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.