Pata taarifa kuu
BURUNDI-AU-USHIRIKIANO-HAKI

Burundi: AU matatani baada ya kutolewa hukumu ya kifungo cha maisha dhidi ya Pierre Buyoya

Hukumu ya kifungo cha maisha dhidi ya Rais wa zamani wa Burundi Pierre Buyoya iliyotolewa mapema wiki hii na mahakama nchini Burundi imeuweka matatani Umoja wa Afrika.

Rais wa zamani wa Burundi Pierre Buyoya, mwakilishi mkuu wa Umoja wa Afrika nchini Mali na katika kanda ya Sahel, kwenye makao makuu ya Umoja wa Ulaya kwenye Umoja wa Mataifa huko Geneva Aprili 1, 2015.
Rais wa zamani wa Burundi Pierre Buyoya, mwakilishi mkuu wa Umoja wa Afrika nchini Mali na katika kanda ya Sahel, kwenye makao makuu ya Umoja wa Ulaya kwenye Umoja wa Mataifa huko Geneva Aprili 1, 2015. AP Photo/Keystone, Salvatore Di Nolfi
Matangazo ya kibiashara

Pierre Buyoya ni mwakilishi mkuu wa Umoja wa Afrika nchini Mali na katika kanda ya Sahel. Umoja aw Afrika haujatoa tangazo lolote kuhusiana na hukumu hiyo, wakati uhusiano unaendelea kudorora kati ya umoja huo na Gitega.

Miaka miwili iliyopita, Umoja wa Afrika ulizungumzia kuhusu suala la waranti wa kimataifa wa kukamatwa uliotolewa na serikali ya Burundi dhidi ya Pierre Buyoya na washtakiwa wenzake, ukiitaka serikali ya Burundi "kujiepusha na hatua yoyote inayoweza kuleta ugumu katika utaftaji wa 'suluhisho la maelewano' nchini.

Waranti huo wa kukamatwa haukuwa na athari kwa rais wa zamani wa Burundi, ambaye sasa ni Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Afrika huko Mali na kanda ya Sahel. Ameeendelea shughuli zake na kusafiri ulimwenguni, kana kwamba hakuna kitu kilichotokea.

Wakati huo huo Pierre Buyoya ameipuuzilia mbali kesi hiyo akisema ilichochewa kisiasa

Pierre Buyoya, ambaye aliongoza Burundi mara mbili na ambaye kila wakati alikabidhi madaraka kwa raia, ni mmoja wa watu mashuhuri wa barani Afrika anayeheshimiwa katika taasisi za kimataifa, licha ya mauaji ya kikabila yaliyoweka dosari katika utawala wake. Hukumu ya kifungo cha maisha dhidi yake inahusiana na mauaji ya Melchior Ndadaye, rais wa kwanza kutoka jamii ya Wahutu aliyechaguliwa kidemokrasia mwaka 1993.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.