Pata taarifa kuu
RWANDA-RUSESABAGINA-HAKI

Mpinzani wa Rwanda Paul Rusesabagina asalia jela

Mahakama ya Rwanda kwa mara nyingine imekataa ombi la kumuachiliwa kwa dhamana Paul Rusesabagina, anayejulikana kwa kuokoa maisha ya watu wengi wakati wa mauaji dhidi ya Watutsi na Wahutu wenye msimamo wa wastani.

Mpinzani wa Rwanda Paul Rusesabagina (katikati) akiwa na wakili wake David Rugaza (kulia) katika mahakama ya Nyarugenge huko Kigali, Oktoba 2, 2020.
Mpinzani wa Rwanda Paul Rusesabagina (katikati) akiwa na wakili wake David Rugaza (kulia) katika mahakama ya Nyarugenge huko Kigali, Oktoba 2, 2020. AFP/Simon Wohlfahrt
Matangazo ya kibiashara

Mpinzani huyu wa Rais Paul Kagame anakabiliwa na mashtaka 13, yote yakihusishwa na vitendo vya ugaidi.

Mahakama imeamua kwamba Paul Rusesabagina anaweza kutoroka nchi ikiwa ataachiliwa, kwa hivyo imefutilia mbali rufaa dhidi ya ombi lake la dhamana.

Jaji pia alijibu hoja kadhaa zilizotolewa na upande wa utetezi, na pia familia ya Paul Rusesabagina, ambao wamebaini kwamba angelishtakiwa nchini Ubelgiji kwa sababu ya uraia wake wa Ubelgiji.

"Alizaliwa Mnyarwanda na hajapoteza uraia wake, kwa sababu inahitaji utaratibu wa kisheria", amesema jaji huyo, pia akibaini kwamba mahakama ya Rwanda ina uwezo wa kushugulikia kesi kwani uhalifu huo ulifanyike nchini Rwanda.

Paul Rusesabagina anahusishwa katika mashambulizi yaliyotekelezwa na kundi la FLN, tawi la kijeshi la kundi la MRCD, muungano wa vyama vya kisiasa vilivyo uhamishoni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.