Pata taarifa kuu
UGANDA-CORONA-AFYA

Uganda yaendelea kulegeza vizuizi dhidi ya Corona

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza kuwa shule na taaissi zingine za elimu ya juu, zitafunguliwa tena kuanzia mwezi ujao. Hatua hiyo inakuja wakati Uganda kufikia sasa imerekodi visa 5,380 vya maambukizi ya virusi vya Corona.

Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni.
Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni. Capture d'écran al-Jazeera
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo wanafunzi Milioni 1.2 walioko kwenye madarasa ya mwisho ya kufanya mitihani ndio watakaoruhusiwa kurejea tena shuleni, baada ya serikali nchini humo kulegeza zaidi ya masharti ya kupambana na janga la Corona.

Museveni amesema wanafunzi hao watarejea shuleni kuanzia tarehe 15 Oktoba, na mikakati imewekwa kuhakikisha kuwa wanakuwa salama.

Shule zilifungwa nchini humo mwezi Machi baada ya kuzuka kwa janga hilo ambalo limewaambukiza watu 6,287 na wengiene 63 kupoteza maisha.

Virusi vya Corona ni jamii kubwa ya virusi vinavyojulikana kusababisha magonjwa yanayoanzia homa ya kawaida hadi homa kali kama vile Homa Kali ya Upumuaji ya Mashariki ya Kati (MERS) na Homa Kali ya Mfumo wa Upumuaji (SARS).

Virusi vipya vya Corona (COVID-19) viligunduliwa 2019 huko Wuhan, China. Hivi ni virusi vipya vya Corona ambavyo havijatambuliwa hapo awali kwa wanadamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.