Pata taarifa kuu
RWANDA-RUSESABAGINA-HAKI

Rwanda: Kesi ya Paul Rusesabagina yafikishwa kwenye ofisi ya mashitaka

Ofisi ya mashtaka ya umma nchini Rwanda, imepokea kesi ya mshukiwa wa ugaidi Paul Rusesabagina na sasa ina siku tano kumwasilisha mahakamani kwa mujibu wa sheria ya kupambana na ugaidi nchini humo.

Paul Rusesabagina amekuwa akihusishwa kushirikiana na kundi la FNL ambalo mwaka 2018 lilishambulia Kusini mwa nchi hiyo karibu na nchi jirani ya Burundi.
Paul Rusesabagina amekuwa akihusishwa kushirikiana na kundi la FNL ambalo mwaka 2018 lilishambulia Kusini mwa nchi hiyo karibu na nchi jirani ya Burundi. NICOLAS MAETERLINCK / BELGA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Rusesabagina anakabilwa na mashataka kadhaa ikiwemo ugaidi, utekaji nyara na mauaji, ambapo anadaiwa kuhusika na mashambulizi yaliopelekea kuuawa kwa raia wasio na hatia na alikamatwa hivi karibuni baada ya kurejea nchini humo akitokea Dubai.

Mazingira ya kukamatwa kwake hayajulikani, lakini polisi ya Rwanda inadai kuwa alikamatwa kutokana na "ushirikiano wa kimataifa". Habari hiyo imethibitishwa na idara ya Upelelezi ya Rwanda (Rwanda Investigation Bureau) kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Wakati wa mauaji ya kimbari, Paul Rusesabagina aliwaokoa mamia ya watu wengi kutoka jamii za Watutsi na Wahutu kwenye hoteli yake ya Mille Collines.

Mapema wiki hii rais wa Rwanda Paul Kagame, alikanusha kuwa serikali yake ilimteka mpinzani wake Paul Rusesabagina, jijini Dubai na kumrudisha nyumbani ili kufunguliwa mashtaka ya ugaidi na mauaji.

Kagame alisema Rusesabagina huenda alidandanywa na kuja nchini Rwanda, hatua iliyopelekea kukamatwa kwake na hakutekwa kama Familia yake inavyodai.

Rusesabagina amekuwa akihusishwa kushirikiana na kundi la FNL ambalo mwaka 2018 lilishambulia Kusini mwa nchi hiyo karibu na nchi jirani ya Burundi.

Kwa zaidi ya miaka 10, Paul Rusesabagina alikuwa mpinzani wa utawala wa Kigali na aliishi kati ya Ubelgiji na Marekani. Tangu muhula wa 3 wa Paul Kagame, chama chake kiliamini kuwa njia ya mtuto wa bunduki ndio itawezesha kupindua utawala wa rais wa sasa Paul Kagame.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.