Pata taarifa kuu
KENYA-CORONA-AFYA

Maambukizi ya virusi vya Corona yakaribia 27,000 Kenya

Visa vya maambukizi ya Corona nchini Kenya, vinakaribia Elfu 27 baada ya watu wengine 492 kuambukizwa katika muda wa saa 24 zilizopita. Wakati huo huo idadi ya vifo imefikia 423 na wagonjwa 13,495 wamepona ugonjwa huo hatari.

Afisa wa afya akinynyuzia dawa kwenye moja ya mitaa huko Nairobi, Mei 15, 2020 (picha ya kumbukumbu)
Afisa wa afya akinynyuzia dawa kwenye moja ya mitaa huko Nairobi, Mei 15, 2020 (picha ya kumbukumbu) REUTERS/Njeri Mwangi
Matangazo ya kibiashara

Watu wengine watatu wamefariki dunia, na kufikisha idadi ya watu waliopoteza maisha kufikia 423 tangu kuanza kwa janga hilo mwezi Machi.

Waziri wa Afya nchini humo Mutahi Kagwe ameendelea kuwataka raia wa nchi hiyo kuendelea kuchukua tahadhari kuzuia maambukizi haya.

Wakati nchi hiyo ikiendelea kukabiliana na janga hilo, Wizara ya afya imeendelea kupata shinikizo za kuweka wazi kuhusu namna inavyotumia fedha za kukabiliana na janga hilo.

Virusi vya Corona vilibainika kwa mara ya kwanza katika mji wa Wuhan katikati mwa China, mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka jana, na vimehusishwa na soko la jumla la vyakula, ambako wanyama wa porini wanauzwa.

Hivi karibuni shirika la Afya Duniani, WHO, lilionya kuwa licha ya jitihada zinazofanyika kutafuta chanjo na dawa ya kupambana na janga la virusi vya Corona, huenda kusiwe na suluhu ya muda mrefu ya kukabiliana na janga hili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.