Pata taarifa kuu
EAC-MKAPA-USHIRIKIANO

Jumuiya ya Afrika Mashariki yaomboleza kifo cha rais Mstaafu Benjamin Mkapa

Bembendera za Jumuiya ya Afrika Mashariki katika nchi wanachama wa jumuiya hiyo zinapepea nusu mlingoti kufuatia kifo cha aliyekuwa rais wa Tanzania Benjamin Mkapa.

Picha ya zamani inayonyesha Rais wa zamani wa Tanzania Benjamin Mkapa.
Picha ya zamani inayonyesha Rais wa zamani wa Tanzania Benjamin Mkapa. © MWANZO MILLINGA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hayati rais mtaafu wa Tanzania Benjamin William Mkapa atazikwa kijijini kwake Lupaso, wilaya ya Masasi mkoani Mtwara, Kusini mwa Tanzania, serikali ya nchi hiyo imetangaza.

Shughuli za kumuaga mzee Mkapa zitafanyika kwa siku tatu mfululizo kuanzia tarehe 26 mpaka tarehe 28, kuanzia Jumapili mpaka Jumanne.

Rais Mkapa ambaye katika utawala wake, alisifika kwa kauli mbiu ya uwazi na ukweli atazikwa Jumatano mchana katika kijiji alikoanzia maisha cha Lupato wilaya ya Masasi., mkoani Mtwara.

Kifo cha rais huyo za wa zamani aliyekuwa na umri wa miaka 81 na aliyeongoza nchi hiyo kati ya mwaka 1995-2005, kilitangazwa na rais John Magufuli.

Aidha, Magufuli alitangaza siku saba za maombolezi, na katika kipindi hicho chote, bendera nchini humo zitapepea nusu mlingoti.

Mkapa, rais wa awamu ya tatu wa Tanzania, atakumbukwa kwa juhudi zake za kusuluhisha migogoro ya kisiasa katika nchi jirani wakati alipokuwa madarakani na hata baada ya kustaafu.

Baada ya machafuko ya baada ya Uchaguzi Mkuu nchini Kenya mwaka 2007, yeye pamoja na Hayati Koffi Annan aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, pamoja na Gracia Machel walisaidia upatikanaji wa maridhiano ya kisiasa nchini humo.

Aidha, alishiriki pakubwa sana katika mazungumzo ya amani ya kisiasa ya Burundi mwaka 2016 yaliyokuwa yanafanyika mjini Arusha.

Kifo chake kimetokea wakati taifa hilo linapoelekea kwenye Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba.

Pamoja na mambo mengine, Watanzania watamkumbuka kwa kuhimiza wawekezaji kutoka nje kuja nchini humo kusaidia kuimarisha uchumi wa taifa hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.