Pata taarifa kuu
KENYA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Idadi ya maambukizi yapindukia zaidi ya 10,000 Kenya

Kenya sasa ina maambukizi zaidi ya Elfu 10 ya virusi vya Corona, baada ya watu wengine 379 kuambukizwa kwa muda wa saa 24 zilizopita na kufikisha idadi ya maambukizi hayo kufikia 10,105.

Kenya inaendelea kukumbwa na maambukizi zaidi.
Kenya inaendelea kukumbwa na maambukizi zaidi. REUTERS/Jackson Njehia
Matangazo ya kibiashara

Awali Wizara ya Afya ilikuwa imebashiri kuwa idadi hii ya maambukizi ingetokea mwezi Aprili lakini, inasema haikuwa hivyo kutokana na jitihada za kuzuia maambukizi hayo.

Idadi hiyo imeongezeka wakati huu nchi hiyo ikiwa imefunguwa safari za ndani za ndege zikitarajiwa kuanza siku ya Jumatano wiki hii, lakini pia kufunguliwa kwa maeneo ya kuabudu.

Waziri wa Afya nchini humo Mutahi Kagwe akizungumza hivi karibuni, amesisitiza kuwa jukumu la kujilinda dhidi ya maambukizi hayo sasa lipo mikononi mwa Wakenya wenyewe.

safari za ndani za ndege zikitarajiwa kuanza siku ya Jumatano wiki hii lakini pia kufunguliwa kwa maeneo ya kuabudu.
safari za ndani za ndege zikitarajiwa kuanza siku ya Jumatano wiki hii lakini pia kufunguliwa kwa maeneo ya kuabudu. REUTERS/Baz Ratner
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.