Pata taarifa kuu
OIF-BURUNDI-USHIRIKIANO

Burundi: OIF yakubali kurejesha tena ushirikiano na Burundi

Jumuiya ya Kimataifa ya nchi zinazozungumza Kifaransa, OIF, inatarajia hivi karibuni kuondoa vikwazo dhidi ya Burundi ilivyoiwekea tangu mwaka 2016.

Warundi wanasubiri kupiga kura katika uchaguzi mkuu huko Ngozi, Jumatano Mei 20, 2020 (picha ya kumbukumbu).
Warundi wanasubiri kupiga kura katika uchaguzi mkuu huko Ngozi, Jumatano Mei 20, 2020 (picha ya kumbukumbu). AFP
Matangazo ya kibiashara

Baraza la Kudumu la jumuiya hiyo, La Francophonie, ambalo linakusanya pamoja nchi wanachama, limesema jana Alhamisi, Julai 9, kuwa liko tayari kwa ombi la serikali ya Gitega kuondoa vikwazo hivyo.

Vikwazo hivyo hivyo vilichukuliwa kufuatia mgogoro uliotokana na uamuzi wa rais wa wakati huo, Pierre Nkurunziza, kuwania muhula wa tatu. Mgogoro ambao hadi mwaka 2017 ulisababisha vifo vya wati 1,200 na kusababisha watu zaidi ya 400,000 kukimbilia uhamishoni.

Katika mahojiano na RFI, mshauri wake katibu mkuu wa Francophonie Bi Vanessa Lamotte, amefahamisha tangu rais mpya wa nchi hiyo Evariste Ndayishimiye aingie madarakani, serikali ya Burundi imeonyesha nia ya kushirikiana na taasisi nyingi za kimataifa,

"Mnamo mwaka wa 2016, Baraza la Kudumu la La Francophonie liliamua kusitisha ushirikiano wa kimataifa na Burundi, kwa sababu ya mambo mbalimbali; vitendo vya dhuluma na pia ukiukwaji wa haki za binadamu.

Kwa hiyo baada ya uchaguzi wa urais uliofanyika mwezi Mei, na kutokana na ombi la serikali ya Burundi Baraza la Kudumu la Francophonie limeamua kwa kauli moja kuiondolea vikwazo nchi hiyo na kurejesha tena ushirikiano, " Mshauri wa katibu mkuu wa OIF, Vanessa Lamothe amesema

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.