Pata taarifa kuu
KENYA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Kenya yaanzisha zoezi la kutoa matibabu kwa wagonjwa nyumba kwa nyumba

Wizara ya Afya nchini Kenya, imezindua mpango wa kutoa matibabu nyumbani kwa wagonjwa wa virusi vya Corona, wakati huu visa vya maambukizi vinaendelea kuongezeka nchini humo.

Watu wakisubiri kufanya vipimo vya virusi vya Corona katika kitongoji cha Kawangware huko Nairobi.
Watu wakisubiri kufanya vipimo vya virusi vya Corona katika kitongoji cha Kawangware huko Nairobi. AFP / LUIS TATO
Matangazo ya kibiashara

Katibu katika Wizara hiyo Rashid Aman amesema asilimia 78 ya watu waliombukizwa virusi hivyo wanaweza kutibiwa nyumbani kwa sababu hawana dalili za virusi hivyo.

Katika hatua nyingine, kwa muda wa saa 24 zilizopita, idadi ya watu waliopona imeongezeka huku idadi walioambukizwa ikiongezeka na kufikia zaidi ya Elfu tatu, baada ya watu wengine 105 kupatikana na virusi hivyo.

Kufikia sasa Kenya imerekodi visa 3,094 vya maambukizi ya virisi vya Corona, ugonjwa ambao umesababisha vifo vya watu 89 na wagonjwa 1,048 wamepona ugonjwa huo hatari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.