Pata taarifa kuu
BURUNDI-NKURUNZIZA-SIASA-USALAMA

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza afariki dunia

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amefariki dunia, Serikali ya nchi hiyo imetangaza katika taarifa yake, siku tatau baada ya kulazwa katika hospitali ya mkoani Karuzi.

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza Juni 7, 2018.
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza Juni 7, 2018. REUTERS/Evrard Ngendakumana
Matangazo ya kibiashara

Nkurunziza alilazwa hospitali ya mkoani Karusi katikati mwa nchi tangu Jumamosi jioni baada ya kujihisi vibaya. Pierre Nkurunziza, ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 2005, inasemekana alifariki jana Jumatatu kufuatia "maradhi ya moyo", taarifa hiyo ya serikali imebaini.

Serikali ya Burundi imetangaza siku 7 za maombolezo ya kitaifa.

Uvumi kuhusu taarifa ya kifo chake ulizagaa tangu Jumatatu mchana. vyanzo vya hospitali vinabaini kwamba alikuwa ameambukizwa virusi vya Covid-19.

Hayo ni wakati mkewe rais Nkurunziza, Denise Bucumi akiendelea kulazwa hospitali nchini Kenya tangu wiki wiki iliyopita baada ya kuambukizwa virusi vya Corona, licha ya viongozi kupuuzia madai hayo.

Pierre Nkurunziza alitarajiwa kukabidhi madaraka kwa rais mpya aliyechaguliwa, Evariste Ndayishimiye, mwezi Agosti.

Taarifa zaidi zitafuata

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.