Pata taarifa kuu
RWANDA--ICC-BIZIMANA-HAKI

Kifo cha Bizimana, mmoja wa washukiwa wakuu wa mauaji ya kimbari Rwanda chathibitishwa

Mabaki ya Augustin Bizimana, mmoja wa washukiwa wakuu wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda mwaka 1994, yamepatikana nchini Congo Brazzaville.

Jumba la Ukumbusho wa mauaji ya Kimbari ya Rwanda huko Kigali.
Jumba la Ukumbusho wa mauaji ya Kimbari ya Rwanda huko Kigali. AFP PHOTO / SIMON MAINA
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa mashtaka katika Mahakama ya Umoja wa Mataifa, amethibitisha hilo na kusema vipimo vya vinasaba vimebaini kuwa mabaki yaliyopatikana ni ya Augustin Bizimana.

Matokeo ya uchunguzi huo, yameonesha kuwa, Bizimana alifariki dunia miaka 20 iliyopita lakini haikuelezwa ni vipi alifariki dunia.

Wakati wa mauaji hayo ya kimbari, alikuwa Waziri wa Ulinzi, wakati watu zaidi ya 800,000 walipouawa kwa muda wa siku 100.

Tangu mwaka 1998, alikuwa anatafutwa na Mahakama ya Umoja wa Mataifa kufunguliwa mashtaka 13 ikiwa ni pamoja na mauaji ya halaiki, mateso na ubakaji.

Hii inakuja, baada ya mshukiwa mwingine wa mauaji hayo Félicien Kabuga kukamatwa nchini Ufaransa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.