Pata taarifa kuu
TANZANIA-KENYA-CORONa-UCHUMI-USHIRIKIANO

John Magufuli: Tumekubaliana kutatua mvutano uliojitokeza mpakani

Rais wa Tanzania Dakta John Magufuli amesema wamezungumza na rais wa Kenya Uhuru Kenya namna ya kutatua mgogoro wa ufungaji wa mpaka baina ya nchi hizo mbili.

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli wamewaachia mawaziri wa Uchukuzi wa Tanzania na Kenya pamoja na Wakuu wa Mikoa kwenye mipaka wamalize matatizo yamliyojitokeza.
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli wamewaachia mawaziri wa Uchukuzi wa Tanzania na Kenya pamoja na Wakuu wa Mikoa kwenye mipaka wamalize matatizo yamliyojitokeza. REUTERS/Sadi Said
Matangazo ya kibiashara

Hatua hiyo inakuja siku chache baada ya nchi ya Kenya kutangaza kufunga mpaka wake na Tanzania katika kudhibiti maambukizi mapya ya virusi vya Corona, hali iliyopelekea Wakuu wa Mikoa iliyo mipakani na Kenya kutangaza kuchukua hatua za kuzuia magari yanayotoka nchini Kenya kuingia nchini Tanzania.

Rais Magufuli amesema baada ya kuongea kwa simu na Rais Kenyata wamekubaliana kutatua mvutano uliojitokeza mpakani.

“Kwa hiyo tumewaachia Waziri wa Uchukuzi wa Tanzania na Waziri wa Uchukuzi wa Kenya pamoja na Wakuu wa Mikoa kwenye mipaka wayamalize haya matatizo. Haya matatizo ni madogo ili kusudi wa Kenya wafanye biashara na wa Tanzania wafanye bishara, “ amesema rais wa Tanzania.

Siku chache zilizopita kwenye mpaka wa Horohoro jijini Tanga, Mkuu wa Mkoa huo Martin Shegela alipiga marufuku magari kutoka Kenya kuingia nchini Tanzania isipokuwa yanayovuka kwenda nchi jirani na yawe na madereva kutoka nchi hizo.

“Kwa gari lolote linalokwenda Rwanda, kwa gari lolote linalokwenda Zambia, Malawi, DR Congo au Uganda inapita ndani ya mpaka wetu waruhusuni waje, ” amesema Martin Shegela.

Mkoani Kilimanjaro Mkuu wa Mkoa huo, Anna Mghwira alisema Magari ya Kenya yataishia kwenye mpaka wa Namanga, mizigo iliyobebwa itafaulishwa na kupakiwa katika magari ya Tanzania.

Mkoani Mara kwenye mpaka wa Sirari, Mkuu wa Mkoa huo Adam Malima alisema wafanyabiashara wanalioingia nchini Kenya walinyanyaswa sasa atachukua hatua za kulipiza kisasi.

“Mimi nachosema tusiende lakini kama na ninyi mna ushahidi kwamba wao wamekuja kwenu siku hiyo mtawaambia polisi ndio hao hapo, mtasema, “ amesema Adam Malima.

Akitetea hatua ya Kenya kufunga mpaka wake na Tanzania, Balozi wa Kenya nchini Tanzania Dan Kazungu amesema adui ni virusi vya Corona, lengo ni kuhakikisha havivuki mpaka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.