Pata taarifa kuu
RWANDA-UFARANSA-ICC-KABUGA-HAKI

Félicien Kabuga afikishwa mbele ya Mwendesha mashtaka jijini Paris

Mtuhumiwa mkuu wa mauji ya Kimbari nchini Rwanda ambaye alikuwa mafichoni kabla ya kukamatwa wiki iliyopita nchini Ufransa, Felicien Kabuga, anatarajiwa kupanda Mahakamani jijini Paris.

Félicien Kabuga alikamatwa nyumbani kwake Jumamosi hii, Mei 16, 2020 huko Asnières-sur-Seine, moja ya vitongoji vya mji w Paris, Ufaransa.
Félicien Kabuga alikamatwa nyumbani kwake Jumamosi hii, Mei 16, 2020 huko Asnières-sur-Seine, moja ya vitongoji vya mji w Paris, Ufaransa. AFP Photos/François Guillot
Matangazo ya kibiashara

Mfadhili huyo wa mauaji ya kimbari yaliyotokea Rwanda mwaka 1994 amefikishwa mbele ya Mwendesha mashitaka mkuu jijini Paris Jumanne wiki hii.

Mahakama ya Paris itaamua iwapo itamkabidhi Kabuga katika Mahakama maalum ya Kimataifa ambayo ilichukua nafasi ya ile iliyokuwa inashughulikia kesi za Kimbari nchini Rwanda iliyokuwa mjini Arusha nchini Tanzania.

Félicien Kabuga alitarajiwa leo Jumatano kusikilizwa na majaji. Lakini kwa ombi la wakili wake, Emmanuel Altit, zoezi hilo limeahirishwa hadi Jumatano ya wiki ijayo. Majaji watakuwa na siku 15 za kuamua juu ya uhalali wa waranti ya kukamatwa iliyotolewa na Mahakama Maalum ya Kimataifa ya IRMCT, mahakama ambayo ina majukumu ya kukamilisha kazi ya mahakama iliyokuwa inashughulikia kesi za Kimbari nchini Rwanda iliyokuwa mjini Arusha nchini Tanzania. Ikiwa waranti hiyo itachukuliwa kuwa ni halali, Félicien Kabuga atapata fursa ya kukata rufaa katika kitengo cha mahakama kuu, ambacho kitakuwa na miezi miwili ya kutoa uamuzi.

Kesi yake kesi yake huenda ikashughulikiwa huko Hague au jijini Arusha, nchini Tanzania.

Félicien Kabuga mwenye umri wa miaka 84, alikamatwa Jumamosi asubuhi huko Asnières-sur-Seine katika moja ya vitongoji wa mji wa Paris, nchini Ufaransa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.