Pata taarifa kuu
RWANDA-MAJANGA YA ASILI

Watu 72 wangamia kufuatia mvua zilizonyesha Rwanda

Watu 72 wamepoteza maisha kutokana na mafuriko ambayo yamesababishwa na  mvua isiyoyakawaida inayoendelea kunyesha nchini Rwanda. Vifo hivyo vimetokea ndani ya saa zisizozidi 12.

Kigali, mji mkuu wa Rwanda, mojawapo ya nchi za Afrika mashariki na Kati zinazoendelea kukumbwa na mafuriko.
Kigali, mji mkuu wa Rwanda, mojawapo ya nchi za Afrika mashariki na Kati zinazoendelea kukumbwa na mafuriko. RFI/Laure Broulard
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa mwandishi wetu nchini Rwanda Bonaventure Cyubahiro mvua hiyo ambayo imekuwa ikiendelea kunyesha imesababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi nchini humo.

Mbali na vifo hivyo, mvua hiyo imeharibu ekari kadhaa za mashamba ya mazao mbalimbali, miundombinu ya kijamii na pia mvua hiyo imevunja madaraja na hivyo mawasiliano kati ya kigali, Gakenke hadi wilayani Musanze yenye vivutio vya utalii yamekata pamoja na maeneo mengine ya nchi mawasiliano yamekata pia. wakazi wa maeneo hayo wamepigwa na bumbu wazi.

Mvua imenyesha kuanzia saa tatu usiku hadi saa kumi na mbili asubuhi, mvua inaponyesha huwa kuna mito inatitiririsha maji kutoka milimani kwenda Mto Sebeya, mto huo unapojaa huanza kusambaza maji mitaani na kusababisha maafa, kwa mujibu wa mwandishi wa RFI Idhaa ya Kiswahili.

Sio mara ya kwanza maeneo hayo kukumbwa na mafuriko, ila safari hii yamezidi mno, ni mafuriko ambayo yamesababisha mawasiliano kukata na watu wameshindwa kutoka sehemu moja hadi nyingine.

Kwa upande wa serikali, Waziri wa Majanga na Shughuli za Dharura Kayisire Marie Solange amesema ni lazima watarekebisha mpango wa kupambana na majanga.

“Mvua ilionyesha ilikuwa nyingi mno, hata sisi tulishangaa kuona sehemu ambazo tulifikia ni zuri zilikabiliwa na mafuriko, ndiyo sababu ttulazimika kukarabati mpango wa kupambana na majanga, hasa mvua” , amesema Bi. Kayisire.

Kwa muda wa wiki tatu, watu wengi walilazimika kuyahama makazi yao kwa kuhofia usalama wao kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.