Pata taarifa kuu
TANZANIA-CORONA-AFYA

Tanzania yatangaza visa vipya 196 vya maambukizi ya virusi vya Corona

Tanzania sasa inaongoza kwa idadi kubwa ya visa vya maambukizi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, ikiwa na jumla ya visa 480 baada ya visa 196 kuthibitishwa nchini humo.

Mji wa kibiashara wa Tanzania, Dar es Salaam, sasa ni kitovu cha maambukizi ya virusi vya Corona.
Mji wa kibiashara wa Tanzania, Dar es Salaam, sasa ni kitovu cha maambukizi ya virusi vya Corona. Wikimedia/Chen Hualin
Matangazo ya kibiashara

Kati ya wagonjwa hao wapya 196, 174 wanatoka Tanzania Bara huku 22 wakitoka kisiwani Zanzibar, kulingana na tayari taarifa ya waziri wa Afya wa visiwa hivyo siku ya Jumanne.

Mji wa kibiashara wa Tanzania, Dar es Salaam sasa ni kitovu cha maambukizi ya virusi vya Corona.

Akizungumza na vyombo vya habari Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa ametangaza ongezeko la wagonjwa 196 wa virusi vya corona, huku akibaini kwamba idadi ya vifo imefikia 16 baada ya ongezeko la watu 6.

Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki zinaendelea kukabiliana na ugonjwa wa Covid-19, huku maambukizi ya virusi vya Corona yakiendelea kuongezeka katika nchi hizo.

Kufikia sasa katika Afrika Mashariki, Tanzania inaongoza kwa wagonjwa 480 ikifuatiwa na Kenya yenye wagonjwa 374, Rwanda zaidi ya 200, Uganda 79, Sudani Kusini zaidi ya 30 na Burundi zaidi ya 10.

Hivi karibuni Shirika la Afya Duniani, WHO, lilikosoa Tanzania kwa kuchelewa kuchukua hatua za mapema kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa huo.

Mpaka sasa Tanzania imechukua hatua kadhaa za kudhibiti ugonjwa huo, hata hivyo serikali ilichelewa kuchukuwa hatua zaidi, amesema Bi Matshidiso Moeti, Mkuu wa WHO katika ukanda wa Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.