Pata taarifa kuu
RWANDA-CORONA-AFYA

Rwanda yawataka raia wake kuvaa barakoa

Kuanzia sasa, kuvaa mask au barakoa ni lazima nchini Rwanda. Mwishoni mwa wiki iliyopita Wizara ya Afya ilitangaza kuwa kuvaa barakoa sasa ni lazima katika maeneo ya umma na katika nyumba ambazo familia kadhaa huishi pamoja.

Muuzaji wa magazeti katika mitaa ya Kigali, Machi 22, 2020.
Muuzaji wa magazeti katika mitaa ya Kigali, Machi 22, 2020. Simon Wohlfahrt / AFP
Matangazo ya kibiashara

Nchi hiyo, ambayo iko katika marufuku ya watu kusalia ndani tangu Machi 22, ina wagonjwa wa Corona 147, na 76 wamepona ugonjwa huo hatari. Mpaka sasa hakuna kifo chochote kinachohusiana na virusi vya Corona ambacho kimeripotiwa nchini humo.

Hatua hiyo inaendelea kutekelezwa vilivyo katika mji mkuu wa Rwanda, Kigali, kwa mujibu wa mwandishi wa RFI, Laure Boulard.

Hata hivyo raia wa Rwanda wanakabiliwa na umaskini, hku wakijiuliza jinsi gani watapata barakoa hizo kwa bei nafuu. Kwa mujibu wa baadhi ya wafanyabiara katika maduka ya dawa, barakoa zinazopatikana nchini Rwanda ni kutoka nchi za kigeni, hususan China, ambazo zinauzwa bei ghali. barakoa moja inauzwa Faranga za Rwanda 1,000 sawa na Euro 1.

Mamlaka nchini Rwanda imebaini kwamba hivi karibuni zitatengenezwa barakoa na kuziuza kwa bei nafuu. Moja itakuwa ikiuzwa Faranga za Rwanda 500, sawa na nusu ya Euro moja.

Mamlaka nchini Rwanda imetoa orodha ya makampuni mengine ishirini yaliyoruhusiwa kutengeneza kile wanachokiita "mask ya kuzuia" kwa bei nafuu. Mask hizo zilianza kutengenezwa tangu Jumatatu wiki hii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.