Pata taarifa kuu
UGANDA-AFYA-CORONA

Coronavirus Uganda: Watu 63 waliofanyiwa vipimo wajikuta hawana virusi

Idadi ya watu walioambukizwa virusi vya Corona nchini Uganda imesalia 44 baada ya  watu 63 waliokuwa wamepimwa  kuthibitishwa hawajaambukizwa. Hata hivyo amri ya kutotoka nje imeendelea kutekelezwa nchini Uganda, huku raia wakilalamikia hatua hiyo.

Amri ya kutotoka nje imeendelea kutekelezwa nchini Uganda, huku raia wakilalamikia hatua hiyo.
Amri ya kutotoka nje imeendelea kutekelezwa nchini Uganda, huku raia wakilalamikia hatua hiyo. REUTERS/James Akena/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya afya kwenye ukarasa wa Twitter hata hivyo imeahidi kutoa taarifa kamili hivi karibuni.

Idadi ya wagonjwa wa virusi vya corona (Covid-19) katika nchi za Uganda na Rwanda imepaa kwa kasi, huku nchi hizo zikipambana kuzuia maambukizi zaidi.

Hivi karibuni Waziri wa Afya wa Uganda, Jane Ruth Aceng aliwaambia wanahabari kuwa nchi hiyo ilibaini wasafiri 2,661 wakiwemo raia wa nchi hiyo ambao wanaweza kuwa na hatari ya kusambaza maambukizi na watu wote hao wapo chini ya uangalizi maaalumu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.