Pata taarifa kuu
KENYA-RWANDA-EU-USHIRIKIANO-UCHUMI

Kenya na Rwanda: Tuko tayari kwa ushirikiano wa kibiashara na Umoja wa Ulaya

Kenya inasema itaanza kutekeleza makubaliano ya kibiashara kati yake na Umoja wa Ulaya, maarufu kama EPA, licha ya mataifa mengine ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, kutokuwa tayari.

Rais wa Rwanda Paul Kagame alipowasili katika Mkutano wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki huko Nairobi Novemba 30, 2012.
Rais wa Rwanda Paul Kagame alipowasili katika Mkutano wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki huko Nairobi Novemba 30, 2012. REUTERS/Noor Khamis
Matangazo ya kibiashara

Mkataba huo wa kibishara ulitarajiwa kuanza kutekelezwa kati ya Umoja wa Ulaya na nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki, lakini ni Kenya na Rwanda ndizo ambazo zimetia saini tayari kuanza ushirikiano huo.

Wanadiplomasia wa Kenya wanasema, kuwa wamekubaliana na Rwanda ili waanze kutekeleza mkataba huo.

Kenya inauza barani Ulaya, Maua, kahawa, chai, mbogamboga na ushirikiano huu unatarajiwa kurahihisha biashara.

Tanzania, Uganda na Burundi wanataka mkataba huo kufanyiwa marekebisho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.