Pata taarifa kuu
AFRIKA MASHARIKI-USALAMA

Jeshi la Pamoja la Afrika Mashariki EASF lashtumiwa

Tangu kuundwa kwa jeshi la Pamoja la Afrika Mashariki EASF mwaka 2005, kwa lengo la kuhimiza amani na usalama wa ukanda na barani Afrika, jeshi hilo halijawahi kwenda katika mataifa yenye mizozo kama Sudan Kusini, Somalia na Burundi.

Askari wasambaratisha umati wa watu katika wilaya ya Cibitoke, Bujumbura, Burundi, Mei 7, 2015.
Askari wasambaratisha umati wa watu katika wilaya ya Cibitoke, Bujumbura, Burundi, Mei 7, 2015. © AP
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa jeshi hilo Dr. Abdillahi Omar Bouh anasema hatua ya jeshi hilo kwenda katika nchi husika ni lazima iamuliwe na Umoja wa Afrika, siku 14 baada ya kuonekana katika nchi husika kuwa hali inakuwa mbaya.

Hata hivyo, Bouh anasema jeshi hilo limekuwa likitoa ushauri kuhusu hai ya usalama nchini Burundi, Sudan Kusini na Somalia.

Wengi wamelishtumu jeshi hilo wakisema kwamba halina jukumu lolote bali limewekwa tu ili kunufaisha baadhi ya watu, hasa viongozi serikalini, huku maafisa wa jeshi hilo wakiendelea kupata mishahara mikubwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.