Pata taarifa kuu
KENYA-MAANDAMANO-UCHAGUZI

Muungano wa upinzani NASA waitisha maandamano makubwa Jumanne hii

Muungano wa upinzani nchini Kenya NASA umeitisha maandamano makubwa nchini kote Jumanne hii kushinikiza maegeuzi ndani ya Tume ya Uchaguzi ikiwa zimesalia siku mbili kabla ya uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika siku ya Alhamisi Oktoba 26.

Maandamano ya upinzani yakitawanywa na polisi ikitumia mabomu ya machozi, Oktoba 6, 2017 Nairobi.
Maandamano ya upinzani yakitawanywa na polisi ikitumia mabomu ya machozi, Oktoba 6, 2017 Nairobi. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa muungano wa upinzani NASA, Raila Odinga, walikuwa na mikutano ya lala salama siku ya Jumatatu.

Akiwa mjini Kisii, Magharibi mwa nchi hiyo, Odinga ambaye ameitisha maandamano ya nchi nzima leo Jumanne kupinga kufanyika kwa uchaguzi huo, amewataka wafuasi wake wasikubali kushiriki katika Uchaguzi huo ambao amesema hautakuwa huru na haki.

Hata hivyo, ujumbe umekuwa tofauti kutoka kwa rais Kenyatta ambaye amekuwa akimalizikia kampeni zake jijini Nairobi baada ya kukutana na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Wafula Chebukati, amewataka wafuasi wake wake kujitokeza kwa wingi kumpigia kura.

Katika hatua nyingine, mgombea wa urais kupitia chama cha Thirdway Alliance, Ekuru Aukot ambaye anaonekena kuwa mshindani mkubwa wa Kenyatta ameimbia Idhaaa ya Kiswahili ya RFI kuwa, ana uhakika wa kushinda uchaguzi huo.

Kwa upande wake, Wizara ya usalama imetoa hakikisho kuwa uchaguzi huo utakuwa salama, huku Polisi wakihimizwa kusimamia sheria na kutotumia nguvu kwa waandamanaji.

Hayo yanajiri wakati ambapo Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi IEBC, Wafula Chebukati, amesema yuko tayari kuwakutanisha Rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga kabla ya uchaguzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.