Pata taarifa kuu
UGANDA

Polisi wamzuia Besigye kuongoza Harambee Chuo Kikuu cha Makerere

Polisi nchini Uganda wamemzuia kiongozi wa chama kikuu cha upinzani FDC Kizza Besigye kuhudhuria mkutano wa Harambee kutafuta pesa kusaidia kufunguliwa tena kwa Chuo Kikuu cha Makerere jijini Kampala.

Kizza Beisgye akiwa ndani ya Lori na ng'ombe aliyekuwa anakwenda kuuza kwenye Harambee Chuo Kikuu cha Makerere jijini Kampala
Kizza Beisgye akiwa ndani ya Lori na ng'ombe aliyekuwa anakwenda kuuza kwenye Harambee Chuo Kikuu cha Makerere jijini Kampala Besigye Twitter
Matangazo ya kibiashara

Besigye ambaye alikuwa amewasilisha ng'ombe wake wenye thamani ya Shilingi za Uganda Milioni 3, amezuiwa kuingia katika eneo la uwanja wa chuo hicho.

Hii sio mara ya kwanza kwa Besigye kuzuiliwa na polisi, siku ya Alhamisi, alizuiwa pia na gari lake kupelekwa nyumbani kwake baada ya maombi katika makao makuu ya chama cha FDC.

Kabla ya mkutano huu, polisi walikuwa wameonya kuhusu kufanyika kwa mkutamo huo kwa madai kuwa ni kinyume na utaratibu kwa sababu Chuo hicho kimefungwa.

Kiongozi wa upinzani Kizza Besigye akizungumza na Polisi baada ya kuzuiliwa kuhudhuria Harambee Chuo Kikuu cha Makerere
Kiongozi wa upinzani Kizza Besigye akizungumza na Polisi baada ya kuzuiliwa kuhudhuria Harambee Chuo Kikuu cha Makerere Kizza Besigye Twitter

Besigye alikuwa ameipa serikali siku 10 kukifungua Chuo hicho la sivyo, ahamasishe watu kuchanga pesa za kuwalipa Wahadhiri.

Serikali ya rais Yoweri Museveni ilifunga chuo hicho baada ya mgomo wa Wahadhiri waliokuwa wamegoma kudai mshahara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.