Pata taarifa kuu
EAC

Rekodi ya haki za binadamu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki yaimarika

Hali ya haki za binadamu katika mataifa ya Ukanda wa Afrika Mashariki imeimarika  katika miaka ya hivi karibuni kinyume na mambo yalivyokuwa  miaka iliyopita, lakini wadau mbalimbali wanastahili kuongeza juhudi za kuimarisha suala hilo. 

Nembo ya haki za binadamu
Nembo ya haki za binadamu cdn.skilledup.com
Matangazo ya kibiashara

Thathmini hii imetolewa na watalaam wa haki za Binadamu wanaokutana kwa siku tatu jijini Dar es salaam nchini Tanzania, kuthathmini hali ya haki za binadamu na namna ya kutatua mizozo katika Mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Hali ya Burundi imeendelea kuwa nzuri baada ya kutokea kwa machafuko ya kisiasa mwaka uliopita, wakati wa maandamano ya kupinga uamuzi wa rais Piere Nkurunziza kuwania urais kwa muhula wa tatu na kusababisha vifo vya mami ya watu na kuwakamata wengine hasa jijini Bujumbura.

Jean Baptiste Baribonekeza Mwenyekiti wa Tume huru ya kutetea haki za binadamu nchini humo ameiambia RFI Kiswahili kuwa, kuna umuhimu wa kufanyika kwa uchunguzi huru ili waliohusika na mauaji ya raia wasiokuwa na hatia wachukuliwe hatua.

Tume ya Haki za Binadamu nchini Uganda nayo inasema hali imeendelea kuwa nzuri tangu mwaka 1986, wakati rais Yoweri Museveni alipoingia madarakani.

Hata hivyo, Dr. Katebalirwe Amooti Kamishena katika Tume hiyo amesema licha ya kuimarika huko, bado kuna changamoto za kisiasa kati ya rais Museveni na kiongozi wa upinzani Kizza Besigye.

Baada ya Uchaguzi wa mwezi Februari mwaka huu na rais Museveni kutangazwa mshindi, Besigye alikataa kutambua matokeo hayo na kutangaza kampeni ya kushawishi raia kususia maswala ya serikali hali ambayo imemsababisha kukamatwa mara kwa mara.

Nchini Kenya, Tume ya Haki nchini humo inataka serikali kuacha kufunga kambi ya wakimbizi ya Daadab ili kuendelea kuheshimu haki za wakimbi kutoka Somalia.

George Morara Naibu Mwenyekiti wa Tume hiyo amesema wamekwenda Mahakamani kuitaka serikali kuachana na mpango huo na kuheshimu sheria za Kimataifa kwa kuwalazimisha wakimbizi hao kurudi nyumbani kwa nguvu.

Watalaam hao pia wanathatmini ni vipi mzozo wa wakulima na wafugaji unaweza kutatuliwa nchini humo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.