Pata taarifa kuu
EAC

Mkutano wa viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waanza jijini Dar es salaam

Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wanakutana jijini Dar es Salaam, nchini Tanzania, huku ajenda kubwa ikiwa ni mazungumzo ya kitaifa ya Burundi na hali ya usalama nchini Sudan Kusini.

Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wanaokutana  jijini Dar es Salaam wakiwa katika picha ya zamani
Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wanaokutana jijini Dar es Salaam wakiwa katika picha ya zamani http://eac.int/
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huu ambao ni wa dhalura, umewakutanisha marais kutoka nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki, mkutano unaofanyika baada ya ule wa baraza la mawaziri wan chi wanachama uliofanyika jijini Arusha siku chache zilizopita.

Wakuu hao wa nchi watapokea taarifa ya mratibu wa mazungumzo ya amani ya Burundi, rais Mstaafu wa Tanzania, Benjamin Mkapa, ambaye ameshakutana kwa zaidi ya mara mbili na wadau wanaohusika na mzozo wa Burundi.

Wakuu hao wan chi wanatarajiwa kuitathmini na pengine kutolea maamuzi baadhi ya masuala ambayo mratibu wa mazungumzo haya atakuwa amewasilisha kwaajili ya kuwa na mazungumzo mengine yatakayopelekea kupatikana kwa suluhu nchini Burundi.

Katika mkutano wake wa mwishono na pande zinazokinzana nchini Burundi, mratibu wa mazungumzo hayo, alionesha kuridhishwa na hatua za awali zilizofikiwa, licha ya kila upande kuonesha unataka kwanza matakawa yake yasikilizwe ili kufikia suluhu.

Muungano wa vyama vya upinzani nchini Burundi wa CENARED, wenyewe ulikataa kushiriki kwenye mazungumzo hayo kwa kile ilichosema ni kutolewa mwaliko kwa chama kimoja kimoja na sio kama muungano.

Upande wa Serikali nao ulidai hautashiriki kwenye mazungumzo hayo kwa kuutaja muungano wa upinzani wa CENARED kuwa kinara wa kuchochea machafuko nchini humo na kwamba ndio uliopanga mapinduzi yaliyoshindikana dhid ya Serikali ya Rais Pierre Nkurunziza.

Mazungumzo haya ni muhimu kwakuwa mbali na kutathmini hali ya mambo nchini Burundi, pia watapokea taarifa kuhus hali ya amani ya nchini Sudan Kusini, safari hii ikiwa imealikwa kama muangalizi kabla ya utiwaji saini wa itifaki kuitambua nchi hiyo kwenye kamati za utendaji za Jumuiya hiyo.

Mwandishi wetu wa Emmanuel Makundi aliyeko kwenye mkutano huo, ameripoti kuwepo kwa mazungumzo ya kina baina ya wadau wa nchi wanachama, huku wazee na watu maarufu barani Afrika na kwenye ukanda wakiwa wamealikwa kuhudhuria.

Mkutano huu pia utatoa hatima ya utiwaji saini wa mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi baina ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya ya umoja Ulaya, mkataba ambao tayari nchi ya Tanzania na Burundi zilisema hazitatia saini hadi pale mazungumzo zaidi yatakapofanyika.

Nchi za Kenya na Rwanda zenyewe zimeshatia saini mkataba huo, huku nchi ya Uganda yenyewe ikieleza utayari wake wa kutia saini mkataba huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.