Pata taarifa kuu
KENYA

Wanaume mjini Mombasa nchini Kenya waanza kufanya uzazi wa mpango

Baadhi ya wanaume mjini Mombasa nchini Kenya wameanza kukumbatia mbinu za kisasa za upangaji uzazi, kama hatua moja ya kuwa na familia bora na zenye mwelekeo thabiti maishani.

Aina ya vidonge vinavyotumika kwa uzazi wa mpango.
Aina ya vidonge vinavyotumika kwa uzazi wa mpango. Photo : Michelle Daniau / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ni hatua ambayo wengi wanaiona kama isiyo ya kawaida kutokana na dhana kuwa wanawake pekee ndi wanafaa kutumia mbinu za kupanga uzazi.

Kuna njia nyingi za kupanga uzazi miongoni mwa wanaume kama vile kutumia mipira ya kondomu kama anavyosimulia Fredrick mkaazi wa Mombasa pwani ya Kenya.

Mwengine ni Joseph Kalume baba wa mtoto mmoja ambaye anasema yeye hutumia njia ya kujiondoa wakati kufanya mapenzi na hivyo hapandi mbegu kwa mkewe.

Wataalam wa afya hapa mjini Mombasa nchini Kenya wanasema ni bora kwa wanandoa kupata ushauri wa njia bora ya kupanga uzazi hasa kwa mwanamke kwa kuwa maumbile yao ni Tofauti.

Liz Kazungu ni muuguzi na mtaalam wa upangaji uzazi katika kituo cha afya cha kibinafsi cha Mikindani medical eneo la mikindani mjini Mombasa, yeye anasema bado elimu haijaeleweka vizuro kwa wananchi kuhusu njia za kupanga uzazi huku wengi wakiwa bado na imani potofu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.