Pata taarifa kuu
SUDAN KUSINI

Ujumbe wa UN kuzuru Juba kushinikiza kutumwa kwa kikosi cha ziada cha askari 4,000 wa kulinda amani

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linapanga kuzuru Sudan Kusini juma lijalo kumshawishi Rais Salva Kiir kukubali kikosi kipya cha kikanda kwa ajili ya kulinda raia la sivyo akabiliwe na vikwazo vya silaha, wanadiplomasia wamesema jana Ijumaa. 

Raia wa Sudani Kusini wakikimbia makazi yao
Raia wa Sudani Kusini wakikimbia makazi yao rfi
Matangazo ya kibiashara

Mabalozi kutoka baraza hilo lenye wanachama 15 wamepanga kusafiri kuanzia Septemba 02 hadi 07 kwa ajili ya mikutano kuhusu mapendekezo ya kupelekwa kwa kikosi cha askari 4,000 mjini Juba kuimarisha kikosi cha Umoja wa Mataifa kinacholinda amani nchini humo kwa sasa.

Kikosi hicho cha umoja wa mataifa UNIMISS kimekosolewa vikali kwa kushindwa Linda raia, ikiwa ni pamoja na wanawake na wasichana kadhaa ambao walibakwa karibu na kambi ya Umoja wa Mataifa mjini Juba baada ya kuzuka kwa vurugu katika mji mkuu Juba mapema mwezi Julai.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.