Pata taarifa kuu
KENYA

Muingereza Jack Marrian aachiwa kwa dhamana, akabiliwa na kifungo cha maisha jela

Mtoto wa mmoja wa viongozi wenye nguvu nchini Uingereza anayekabiliwa na mashtaka ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya Cocaine, zenye thamani ya dola za Marekani milioni 5.8, ameachiwa kwa dhamana baada ya jaji kukataa ombi la upande wa mashtaka kutaka mtuhumiwa huyo aendelee kushikiliwa.

Jack Alexander Wolf Marrian, raia wa Uingereza anayekabiliwa na kesi ya kusafirisha dawa za kulevya nchini Kenya, akiwa mahakamani hivi karibuni
Jack Alexander Wolf Marrian, raia wa Uingereza anayekabiliwa na kesi ya kusafirisha dawa za kulevya nchini Kenya, akiwa mahakamani hivi karibuni DR
Matangazo ya kibiashara

Jack Marrian mwenye umri wa miaka 31, alikamatwa baada ya polisi kwenye mji wa Mombasa, kufanya msako maalumu Julai 29 mwaka huu na kumkuta akiwa na kilo 100 za dawa aina ya Cocaine zilizokuwa zimeagiziwa kama mifuko ya sukari.

Mahakama kuu ya Nairobu imeunga mkono hukumu ya awali iliyotolewa kuruhusu Marrian kuachiwa kwa bondo ya shilingi za Kenya milioni 70 ambayo itadhaminiwa na raia wawili wa Kenya pamoja na kusalimisha pasi yake ya kusafiria.

Jaji aliyekuwa akisikiliza rufaa ya upande wa mwendesha mashata wa Serikali, amesema kuwa, hakushawishika na utetezi wa upande wa mashtaka uliotaka mtuhumiwa huyo aendelee kuzuiliwa kutokana na ukubwa wa kosa linalomkabili.

Mwingine aliyeachiwa huru kwenye shauri hilo, ni raia wa Kenya, Roy Mwanthi ambaye anakabiliwa na mashtaka kama hayo.

Marrian alishtakiwa kwa mara ya kwanza August 4 mwaka huu baada ya polisi wa kimataifa Interpol kupewa taarifa kuhusu mzigo uliokuwa unafuatiliwa na majasusi wa Marekani na wale wa Kenya.

Kesi yake ambayo imevuta hisia za raia wengi wa Uingereza kutokana na historia ya familiya yake na hasa mama yake, Lady Emma Clare Campbell wa Cawdor na kuhudhuria kwake kwenye shule za gharama kubwa kama aliyosoma mke wa Prince Williams, Catherine.

Baba yake, David Marrian amesema anaamini mwanae atasafishwa kutokana na kashfa hiyo, na kwamba anaungwa mkono na muajiriwa wake.

Bandari ya Mombasa, kwa muda mrefu sasa imekuwa kitovu cha upitishaji wa dawa haramu barani Afrika zinazopitishwa kwenda Asia na Ulaya.

Kesi yake imetajwa kuanza kusikilizwa October 3 mwaka huu, ambapo akipatikana na hatia huenda akakabiliwa na kifungo cha maisha jela.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.