Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA

Upinzani nchini Kenya waishtumu serikali kutaka kubomoa demokrasia

Upinzani nchini Kenya, unaishtumu serikali kuwa na mpango wa kurejesha nchi hiyo kwenye enzi za chama kimoja cha KANU.

Kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga
Kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga REUTERS/Noor Khamis
Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa chama cha ODM na aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga, amesema hatua ya vyama vya siasa vinavyoiunga mkono serikali ya rais Uhuru Kenyatta kuamua kuungana na kuunda chama kimoja ni kuua demokrasia ya vyama vingi nchini humo.

“Hii ni mbinu ya kujaribu kuturejesha kwenye utawala wa chama kimoja cha Baba na Mama,” alisema Odinga.

Aidha, amesema kuwa wakenya hawatakubali mbinu hii inayotumiwa na serikali kuelekea uchaguzi Mkuu mwaka ujao.

“Mtoto ameshazaliwa na huwezi kumrudisha tumboni, ukahaba huu wa kisiasa ni lazima ukome,” alisisitiza.

Siku ya Jumanne, rais Kenyatta alitangaza kukamilika kuundwa kwa chama cha Jubilee, kitakachozinduliwa rasmi mwezi ujao jijini Nairobi kuelekea uchaguzi Mkuu mwaka ujao.

Kenyatta alisema kuundwa kwa chama hiki kutasaidia kupambana na siasa za kikanda na kikabila.

Vyama 12 vimekubali kuvunjwa na kuingia kwenye chama kimoja cha JAP, atakachotumia rais Kenyatta kutetea wadhifa wake mwaka ujao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.