Pata taarifa kuu
KENYA-UTAMADUNI

Msimu wa kuwatairi wavulana nchini Kenya waanza

Msimu wa kila mwaka wa kuwatahiri wavulana wenye umri wa miaka 15 katika Kaunti ya Bungoma, Magharibi mwa Kenya imezinduliwa leo.

Wavulana wakiimba muda mfupi kabla ya kwenda kutairiwa katika Kaunti ya Bungoma, Magharibi mwa Kenya
Wavulana wakiimba muda mfupi kabla ya kwenda kutairiwa katika Kaunti ya Bungoma, Magharibi mwa Kenya npr
Matangazo ya kibiashara

Tamaduni hii hukutelezwa na watu wa kabila dogo la Wabukusu ambao wapo ndani ya kabila kubwa la Waluhya.

Mvulana anayetahiriwa anastahili kuonesha ushapavu na kutotoa hata chozi, ishara ambayo Wabukusu wanasema ni ishara ya ushupavu na ukomavu.

Kabla ya kitendo hicho, Shangazi wa mvulana aliyetahiriwa humtishia kumpiga kwa mwiko wa kupikia ugali.

Mvulana anayekwenda jandoni  anatarajiwa kuuzuia ishara ya ushupavu kabla ya kwenda mtoni, kupakwa tope na watu maalum kabla ya shu

Inaaminiwa kuwa baada ya mvulana kupitia kisu cha ngariba anakuwa mwanaume kamili na wakuheshimiwa katika jamii.

Wavulana waliopitia hali hii  huimbiwa nyimbo za kishujaa na kuitwa mwanaume kamili ambaye yupo tayari kuoa na kipindi hicho anastahili kula vizuri na sasa anawajibika kutembea na rika lake.

Hata hivyo, tamaduni hii ya jadi imekuwa ikiimarishwa katika miaka ya hivi karibuni ikiwa ni pamoja na ngariba kutumia visu tofauti kwa wavulana hao lakini pia dawa za kisasa kutumiwa ili kuzuia magonjwa hatari kama Ukimwi.

Wazazi siku hizi pia hawalazimishwi kuwapeleka wanao jandoni kama ilivyokuwa zamani lakini wanaweza kuwapeleka hospitalini.

Utamaduni huu pia umekuwa kivutio cha utalii katika Kaunti hiyo ya Bungoma.

Gavana wa jimbo hilo Ken Lusaka ameahidi kutoka Shilingi za Kenya 5,000 kwa wavulana wanaotoka katika Familia maskini watakaotahiriwa mwezi huu.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.