Pata taarifa kuu
SUDAN KUSINI

Waziri wa Kilimo ajiuzulu, amtaka rais Kiir aachie madaraka

Waziri wa Kilimo nchini Sudan Kusini Lam Akol amejizulu, uamuzi ambao ameuchukua hivi leo akiwa jijini Addis Ababa nchini Ethiopia.

Lam Akol akihojiwa na wanahabari
Lam Akol akihojiwa na wanahabari wordpress.com
Matangazo ya kibiashara

Akol ambaye ni mwanasiasa wa upinzani na mshirika wa zamani wa aliyekuwa Makamu wa kwanza wa urais Riek Machar, amesema amechukua uamuzi huo kuendeleza shinikizo za kumtaka rais Salva Kiir ajiuzulu.

Mwanasiasa huyo ni kiongozi wa chama kingine cha upinzani cha SPLM-DC na baada ya kuchukua uamuzi huo, ameshutumu Machar kwa kushindwa kuthibiti vikosi vyake baada ya mapigano ya hivi karibuni yaliyosababisha zaidi ya watu 300 jijini Juba.

Aidha, ameongeza kuwa kwa sasa hakuna mkataba wowote wa amani wa kutekelezwa na kinachostahili kufanyika kwa sasa ni kujiuzulu kwa rais Kiir ili kupisha serikali mpya.

Machar aliondoka jijini Juba na haijulikani alipo hali ambayo inaendelea kuzua hali ya wasiwasi nchini humo.

Mwezi uliopita, rais Kiir alimteua Jenerali Taban Deng Gai kuwa Makamu wa kwanza rais kuchukua nafasi ya Machar, uteuzi ambao umeshtumiwa na Jumuiya ya Kimataifa na upinzani nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.