Pata taarifa kuu
UGANDA-USALAMA

Watu 8 wauawa na askari katika kambi Uganda

Askari anayesadikiwa kuwa alikua na ugomvi na mkewe aliwaua kwa kuwapiga risasi watu wanane ndani ya kambi ya kijeshi ya Makindye mjini kampala nchini Uganda.

Gari ya jeshi la Uganda ikiegeshwa kwenye mlima wa Rwenzori, karibu na kijiji cha Kichwamba (kusini magharibi mwa Uganda).
Gari ya jeshi la Uganda ikiegeshwa kwenye mlima wa Rwenzori, karibu na kijiji cha Kichwamba (kusini magharibi mwa Uganda). Gaël Grilhot/RFI
Matangazo ya kibiashara

Taarifa hii imethibitishwa na msemaji wa jeshi la Uganda meja Edward Birungi, ambaye amesema kuwa askari huyo anaripotiwa kutofautiana na mkewe.

Pia inasemekana kuwa askari huyo alikua amevuta bangi akiwa kazini. Alianza kurusha risasi kiholela akimtafuta mkewe. Hata hivyo inaarifiwa kuwa mke wa askari huyo alinusurika baada ya kufaulu kutoroka.

Wanawake wanne akiwemo mwanajeshi mmoja ni miongoni mwa watu waliouawa naaskari huyo, ambaye pia aliuawa na askari wenzake.

Wengiwe waliouawa ni pamoja na wake wa wanajeshi wengine, wakiwemo pia watoto watatu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.