Pata taarifa kuu
KENYA-UPINZANI

Uwanja wa Nyayo umepigwa marufuku kutumiwa kwa mikutano

Serikali ya Kenya imepiga marufuku kutumiwa kwa uwanja wa Michezo wa Nyayo na Bustani ya Uhuru kwa mikutano hapo kesho kwa sababu za kiusalama.

Askari polisi akimpiga mmoja wa waandamanaji Nairobi, Kenya Mei 16, 2016.
Askari polisi akimpiga mmoja wa waandamanaji Nairobi, Kenya Mei 16, 2016. REUTERS/Goran Tomasevic
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inakuja baada ya kuzuka kwa mvutano kati ya muungano wa upinzani wa CORD na Shirika moja la kidini kuhusu ni nani aliyestahili kutumia bustani ya Uhuru kesho siku ambayo Kenya inaadhimisha miaka 53 ya Uhuru wa Bendera.

Hata hivyo, upinzani unasema hautatishwa na uamuzi wa serikali na utaendelea na mkutano wake wakati rais Uhuru Kenyatta atakapokuwa anawaongoza raia wa nchi hiyo kuadhimisha siku ya Madaraka katika uwanja wa Afraha mjini Nakuru.

Hali ya kisiasa nchini Kenya imekumbwa katika majuma haya matatu na maandamano katika miji mbalimbali ya Kenya. Upinzani umekua ukiandaman ukitaka wajumbe wa Tume huru ya Uchaguzi waondolewe, ukibaini kwamba hawawajibiki kwa kazi yao.

Hata hivyo, wajumbe hao hivi karibuni wamesema hawatishwi na madai ya upinzani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.